Pamoja na maambukizi ya ugonjwa wa malaria kupumgua kwa
aslimia 40 kutoka wagonjwa million saba mwaka 2015 hadi kufikia
wagonjwa million nne mwaka 2017, bado Mkoa wa Geita ni miongoni mwa
Mikoa minne ambayo kiwango cha maambukizi hakijapungua.
Kutokana na hali hiyo moja ya ujumbe wa mwenge kitaifa mwaka huu ni
kushiriki kutokomeza malaria kwa manufaa ya jamii.
Akiwa wilayani Mbogwe kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Charles
Kabeho alisema pamoja na mafanikio makubwa ya kupunguza maambukizi ya
ugonjwa huo bado tatizo la malaria limeendelea kuwa kubwa.
Takwimu hizo zinaonyesha vifo vimepungua kutoka 6,311 mwaka 2015 hadi
kufikia vifo 5,382 mwaka 2017`na kwamba pamoja na kupungua kwa vifo
bado ugonjwa wa malaria ni tatizo kubwa kwa afya za wananchi.
`
Kabeho aliwataka wananchi kuhamasika na kuona umuhimu wa matumizi ya
viuadudu vya kibailojia katika kuangamiza viluwiluwi vya mbu katika
mazalia yao.
“wananchi tunzeni mazingira kwa kufyeka majani na vichaka kandokando
ya nyumba zenu na kuharibu mazalia yote ambapo maji yametwama ili mbu
wasizaliane “alisema Kabeho
Akizungumza katika kituo cha afya Masumbwe wakati wa zoezi la ugawaji
vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano Muuguzi wa
kituo cha afya Masumbwe Yohana Filipo alisema halmashauri ya Mbogwe
kwa kipindi cha julai 2017 hadi machi 2018 wamegawa vyandarua 23,000
kwa kina mama wajawazito na watoto.
Alisema katika kipindi hicho wananchi 82,000 walipima malaria na kati
yao wananchi 26,961 ambao ni sawa na asilimia 33 walikutwa na vimelea
vya malaria na kwamba mwamko wa wananchi kupima kabla ya kuanza dawa
umesaidia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa waliokuwa wakitumia dawa
bila kupima.
Aidha Mwenge wa Uhuru ulizundua jengo la upasuaji katika kituo cha
afya Iboya. Jengo hilo hadi kukamilika limegharimu shilingi 387,579,734 milioni
Kufunguliwa kwa jengo hilo ni mkombozi kwa kina mama wajawazito
wanaopata shida wakati wa kujifungua na kulazimika kupelekwa kituo cha
afya Masumbwe kupata huduma ya upasuaji.
Mwenge wa uhuru pia uliweka jiwe la msingi barabara ya
Busafya-Nyakasaluma-Kanegere gerezani yenye urefu wa km 10
inayojengwa kwa kiwango cha cahangarawe kwa gharama y a sh,206 milion.
Mwenge wa uhuru ukiwa wilayani Mbogwe ulizindua,kukagua na kufungua
miradi 10 yenye thamani ya sh, 1.1 bilion
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.