Mkuu wa Kitengo
Imelda Gwassa
A: UTANGULIZI:
Kitengo cha Ufugaji nyuki kilianzishwa rasmi Februari, 2016 kikiwa na malengo ya kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao ya nyuki pamoja na kukuza kipato cha wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla wake. Kwa kutambua umuhimu huu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe imeendelea kuhamasisha ufugaji wa nyuki kupitia vikundi na watu binafsi katika kata za Iponya, Masumbwe, Nyakafuru, Bukandwe, Nhomolwa, Lugunga, Mbogwe, Nanda na Ngemo. Takribani watu 410 wanajishughulisha na ufugaji wa nyuki
B:HUDUMA ZITOLEWAZO NA KITENGO CHA UFUGAJI NYUKI:
Ili kukuza na kuendeleza ufugaji bora na wa kisasa wa nyuki, majukumu ya Kitengo hiki ni:
Kuboresha huduma za ugani kwa kutoa elimu ya ufugaji bora wa nyuki kwa wakati
Kuhamasisha na kuanzisha vikundi vya wafugaji nyuki katika Kata au Kijiji
Kutoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira ambayo nyuki watatumia kutengeneza asali
Kuhakikisha njia za urinaji wa asali zinazotumika haziui nyuki wala kuharibu mazalia au masega yao
Kusimamia ubora wa mazao ya nyuki ili kulinda afya ya mtumiaji
Kutengeneza mizinga bora ya mfano kwa ajili ya ufugaji wa nyuki na kufundishia
Kuwezesha upatikanaji rahisi wa zana na vifaa vya kisasa vya kuvunia asali
Kuwatafutia wafugaji soko la uhakika la asali
Kuwasaidia wakulima walioko katika vikundi kuanzisha vituo vya kukusanyia na kuuza asali
Kuanzisha mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki na hifadhi ya mazingira
Kufanya tathmini ya kila mwaka ya ukuaji wa sekta ya ufugaji wa nyuki
Kuwezesha vikundi vya wafugaji wa nyuki kuhudhuria maoneshoya siku ya wakulima nane nane ili kuonesha bidhaa zao katika kanda husika
Kuwashawishi wananchi kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa ili kukuza mitaji
Kutenga maeneo maalum ya ardhi kwa ajili ya wafugaji wa nyuki
Kutoa huduma bora kwa wadau wote kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma.
Kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo za Hifadhi, Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.
C: IKAMA YA WATUMISHI
Kitengo cha ufugaji nyuki kina mtumishi mmoja.
D: TAKWIMU MUHIMU ZA KITENGO
Takwimu zinaonesha kwamba takribani watu 410 wanajishughulisha na ufugaji nyuki. Maeneo muhimu, idadi ya mizinga na vikundi ni kama inavyoonesha katika jedwali:
Na.
|
KATA
|
MIZINGA YA KISASA
|
MIZINGA YA KIENYEJI
|
JUMLA YA MIZINGA
|
JUMLA YA VIKUNDI
|
1
|
MASUMBWE
|
40
|
78
|
118
|
5
|
2
|
IPONYA
|
563
|
18,649
|
19,212
|
3
|
3
|
NYAKAFURU
|
2
|
77
|
79
|
2
|
4
|
NHOMOLWA
|
48
|
70
|
118
|
2
|
5
|
BUKANDWE
|
96
|
230
|
326
|
4
|
6
|
LUGUNGA
|
10
|
0
|
10
|
1
|
7
|
NANDA
|
10
|
207
|
217
|
1
|
8
|
NGEMO
|
22
|
41
|
63
|
0
|
9
|
MBOGWE
|
18
|
504
|
522
|
1
|
|
JUMLA
|
761
|
19,786
|
20,547
|
19
|
E: WAJIBU WA MFUGA NYUKI
Wajibu wa mfuga nyuki ni:
Kutumia mizinga ya kisasa katika ufugaji nyuki
Kurina asali kwa kutumia njia za kisasa badala ya kutumia moshi au moto
Kuhifadhi mazingira kwa kutochoma moto au misitu
Kujiunga katika vikundi vya uhifadhi ya mazingira
Kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa vya wafugaji wa nyuki
Kutumia dawa isiyoua nyuki wala kuharibu ubora wa asali wakati wa urinaji
Kutumia vyombo au vifaa vilivyo safi na salama kwa ajili ya kurinia na kuhifadhia asali
Kuhudhuria mafunzo yatolewayo katika mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki
F: MAKOSA KWA MJIBU WA SHERIA NDOGO ZA HALMASHAURI
Mdau yeyote atakuwa ametenda kosa endapo atafanya mambo yafuatayo:
Atarina asali kwa kutumia moto au moshi
Atauza asali iliyorinwa kwa moto au moshi
Atachanganya au amechanganya asali na vitu vingine ambavyo siyo asali
Atachoma moto msitu au eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya wafugaji wa nyuki
Atakata miti bila kuwa na kibali kutoka Halmashauri
Atang’oa miti iliyopandwa kwa ajili ya kuhifadhi mazinggira
Atatenda jambo lolote ambalo linadhuru au linahatarisha maendeleo na ukuaji wa kilimo cha nyuki
Atatenda kitendo chochote kinachohatarisha upatikanaji wa asali yenye ubora na salama
Atahujumu miundo mbinu ya ufugaji wa nyuki ya shule, kikundi, kijiji, mtaa, kata, taasisi na mtu binafsi
Na akipatikana na hatia chini ya kifungu cha 26 cha sheria Ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, atatozwa faini isiyopungua elfu hamsini (50,000/=) na isiyozidi shilingi laki tatu (300,000/=) au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au vyote viwili yaani kifungo na faini.
G:UWEKEZAJI
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe kwa kushirikiana na TFS walitoa jumla ya mizinga 330 ya kisasa aina ya kati kwa vikundi vya ufugaji nyuki katika kata za Iponya, Masumbwe, Nyakafuru, Nanda, Mbogwe, Lugunga, Nhomolwa, Bukandwe na Ngemo.
Mafundi seremala 10 kutoka kata za Iponya, Mbogwe na Masumbwe walipatiwa mafunzo ya utengenezaji wa mizinga ya kisasa aina ya katiyaliyofanyika Mwanza Oktoba,2015.
H: CHANGAMOTO
Pamoja na mafanikio ya ufugaji nyuki pia zipo changamoto katika sekta hii.
Shughuli za kibinadamu katika maeneo ya ufugaji nyuki kama ukataji miti ovyo kwa ajili ya mkaa, mbao, uchomaji matofali, ukaushaji wa tumbaku na matimba kwa ajili ya kuweka kwenye mashimo ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini, utayarishaji wa mashamba kwa kukata miti na kuchoma moto na Ufugaji wa mifugo kwenye maeneo ya ufugaji nyuki.
Uhaba wa maeneo binafisi ya ufugaji nyuki
Upungufu wa Wataalam wa ufugaji nyuki
I: MIKAKATI YA KUENDELEZA SEKTA YA NYUKI
Mikakati madhubuti inahitajika ili kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki katika utoaji wa huduma bora kwa jamii. Katika kukabiliana na changamoto zilizopo mikakati ifuatayo ni muhimu ikazingatiwa:
Kuendelea kutoa elimu ya hifadhi bora ya mazingira kwa jamii na kufanya doria za mara kwa mara ili kubaini na kuzuia ukataji ovyo wa miti katika maeneo ya ufugaji nyuki
Kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kuwawezesha wafugaji nyuki kuwa na hati miliki ya maeneo ya ufugaji
Kuongeza wataalam wa sekta ya ufugaji nyuki ili kuboresha utoaji wa huduma bora kwa jamii
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.