• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Frequently Asked Questions |
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe

The United Republic of Tanzania MBOGWE DISTRICT COUNCIL MBOGWE DISTRICT COUNCIL

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Administration and human resource
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Finance and Business
      • Social Work
      • Health
      • Ardhi na Mali Asili
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji na Udhibiti Majitaka
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
    • Units
      • Procurement and Supply
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa na Uwekezaji
  • Huduma
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na mazingira
      • Kamati ya Elimu Afya na Maji
  • Miradi
    • Project Projection
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha za Matukio mbalimbali
  • Machapisho
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu mbalimbali

Works and Fire Rescue Department

Mkuu wa Idara

Mhandisi  Robert Kisandu

UTANGULIZI

Idara ya Ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ni Idara muhimu inayochochea maendeleo na kusogeza huduma za jamii kwa wananchi

Idara ya ujenzi ina vitengo vifuatavyo:-

  • Barabara
  • Majengo
  • Mitambo na Magari
  • Umeme na Nishati

SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA

Kusimamia matengenezo ya barabara za vijiji na Wilaya ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.

Kusimamia ujenzi wa barabara mpya za vijiji na Wilaya ili kuongeza urefu wa mtandao wa barabara ndani ya Wilaya.

Kusimamia ujenzi na ukarabati wa Makalavati, Madaraja na Vivuko katika barabara za vijiji na Wilaya ili ziweze kupitika kipindi chote cha mwaka.

Kusimamia ujenzi wa miundombinu ya majengo ya Serikali na binafsi ili yaweze kukidhi ubora wa viwango vinavyotakiwa.

Kusimamia Mitambo na magari ya Serikali chini ya umiliki wa Wilaya.

Kusimamia Nishati na Umeme katika majengo ya Serikali na binafsi.

Kufanya upembuzi yakinifu, usanifu na kutoa ushauri wa shughuli zote za barabara, madaraja na majengo.

Kuandaa ramani, makadirio, Bajeti na mpango kazi wa shughuli zote za barabara, madaraja na majengo

Kuandaa taarifa za kila robo mwaka za utekelezaji wa shughuli zote za barabara, madaraja na majengo

HALI YA WATUMISHI KATIKA IDARA YA UJENZI

  • Idara ya Ujezi ina watumishi 8 hadi sasa ambao mchanganuo wao ni kama ifuatavyo:-
  • Mkuu wa Idara ya Ujenzi (Civil Eng I) – 1.
  • Mhandisi II (Civil Eng II) – 1.
  • Fundi sanifu Mkuu – Barabara (Senior Civil Tech) – 1.
  • Fundi sanifu Mkuu – Usanifu majengo (Senior Architecture Tech) – 1.
  • Fundi sanifu I - Majengo (Tech I) – 1.
  • Fundi sanifu II - Majengo (Tech I) – 2.
  • Dereva - 1

TAKWIMU MUHIMU ZINAZOHUSIANA NA IDARA YA UJENZI

Idara ya Ujenzi katika Wilaya ya Mbogwe inasimamia Mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilometa 822.0 kwa mchanganuo ufuatao:-

  • Barabara za Mijini katika miji midogo ya Masumbwe km 25, Nyakafuru km 35 na Mbogwe km 50.
  • Barabara za Wilaya km 326.7 
  • Barabara za vijijini km 385.3 
  • Hali halisi ya mtandao wa barabara za Wilaya ya Mbogwe ni kama ifuatavyo:-
  • Urefu wa barabara za changarawe ni km 49.4
  • Urefu wa barabara za udongo ni Km 772.6
  • Wilaya ya Mbogwe haina barabara za lami isipokuwa kuna jumla ya km 35 za barabara kuu ya lami kutoka Isaka hadi Lusahunga inayomilikiwa na Wakala wa barabara Mkoa wa Geita (TANROADS).
  • Aidha Wilaya ya Mbogwe ina jumla ya km. 86 za barabara za udongo na changarawe zinazomilikiwa na Mkoa wa Geita (TANROADS).

MIRADI INAYOTEKELEZWA NA IDARA YA UJENZI:

  • Tangu Idara ilipoanzishwa mwaka wa fedha 2013/2014 hadi kufikia mwaka 2016/2017, Idara ya Ujenzi imeweza kujenga na kufanya matengenezo kwa kutumia Wakandarasi, Mafundi na Wananchi katika Miradi ifuatayo:-
  • Idara ya Ujenzi imesimamia ujenzi na matengenezo ya Barabara za Vijiji na Wilaya zenye urefu wa km 476.76 kati ya km 822.0, sawa na 58%.
  • Idara imeweza kusimamia Miradi ya ujenzi wa majengo ya shule ya Sekondari Iponya chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia SEDP II ambayo ujenzi wake umekamilika
  • Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe katika Kijiji cha Kasosobe ambao kwa sasa msingi wa jengo la awamu ya I umekamilika na nguzo za kuanzia zimejengwa, kazi inaendelea.
  • Idara imesimamia ujenzi na ukarabati wa wa miundombinu ya majengo ya shule za Sekondari na Msingi, vituo vya afya, Zahanati, Ofisi za Vijiji na Kata.
  • Idara imeshiriki kikamilifu katika usimamizi wa Miradi ya TASAF III ya malambo matano na ujenzi wa barabara zenye urefu wa km 14.
  • Idara imekuwa ikishauri na kuelekeza kikamilifu Mashirika, Makampuni na Wananchi  katika ujenzi wa miundombinu binafsi ili ijengwe kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu za ujenzi.

BAJETI YA IDARA YA UJENZI - MBOGWE:

  • Jumla ya Tshs 3,328,716,400.00 zinazotokana na Mfuko wa barabara (Road Fund) zilitengwa tangu Idara ilipoanzishwa mwaka wa fedha 2013/2014 hadi kufikia mwaka 2016/2017, Idara ya Ujenzi imekuwa ikipokea fedha za Miradi ya matengenezo na ujenzi wa barabara kutoka Mfuko wa barabara (Road Fund) kama ifuatayo:-
  • Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013/2014 Idara ilitenga Tshs 260,800,000.00.
  • Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 Idara ilitenga Tshs 1,055,010,000.00.
  • Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 Idara ilitenga Tshs 663,946,400.00.
  • Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 Idara ilitenga Tshs 1,348,960,000.00.
  • Fedha hizi zimekuwa zikitumika katika kuimarisha, kuboresha na kuongeza mtandao wa barabara Wilayani Mbogwe kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Wananchi wote.

HUDUMA MUHIMU ZINAZOTOLEWA NA IDARA.

  • Idara ya Ujenzi mara kwa mara huelimisha wananchi kupitia Ofisi za maafisa watendaji wa Vijiji vyote, maafisa watendaji wa Kata zote, Maafisa Tarafa wote na Madiwani wote waliopo ndani ya Wilaya namna ya wananchi kulinda, kutunza na kuwa na matumizi yaliyo sahihi kwenye miundombinu ya barabara na majengo ya Serikali.
  •  
  • Huduma ya uelimishaji, ushauri na uelekezaji juu ya miundombinu ya barabara na majengo hupatikana siku zote za kazi katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kupitia Ofisi ya Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya ya Mbogwe.

TAARIFA MUHIMU KWA WANANCHI.

  • Wakati wa ujenzi na matengenezo ya Miundombinu ya barabara na majengo Idara ya Ujenzi huelimisha wananchi, vibarua na mafundi juu ya kuhakikisha usafi unazingatiwa ikiwa ni pamoja na kutumia maji safi na salama na kujenga vyoo vya muda na tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa kuepuka maambukizi ya magonjwa ikiwa ni pamoja na HIV (UKIMWI)


Announcements

  • Watoto wa kike waliokatisha Masomo yao November 01, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA USAJILI WA ANWANI ZA MAKAZI March 09, 2022
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi kwa Walimu September 06, 2020
  • Ratiba ya Kampeni za Kampeni Jimbo la Mbogwe August 26, 2020
  • View All

Latest News

  • Progamu ya utoaji wa Chakula Mashuleni wilayani Mbogwe

    May 20, 2022
  • Maadhimisho ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

    April 26, 2022
  • Maadhimisho ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

    April 26, 2022
  • Mkurugenzi Mtendaji Bi Saada Selemani Mwaruka katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

    April 26, 2022
  • View All

Video

UFUNGUZI WA MAJENGO MAPYA NA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA CHA MASUMBWE, GEITA
More Videos

Quick Links

  • MKOA WA GEITA
  • WIZARA YA TAMISEMI
  • IKULU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  • MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA)
  • BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA(NECTA)
  • WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
  • WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TKNOLOJIA
  • WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Related Links

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora
  • Mkoa wa Geita

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita

    Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe

    Telephone: +255734412592

    Mobile: +255734412592

    Email: ded@mbogwedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.