NAIBU WAZIRI WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA ,WAZEE NA WATOTO, MH KHAMIS KIGWANGALA AMEFANYA ZIARA KWENYE KITUO CHA AFYA MASUMBWE, MBOGWE.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto amefanya ziara kwenye kituo cha Afya Masumbwe na kujionea jinsi kituo hicho kinavyotoa huduma kwa jamii. Katika ziara hiyo Mh kigwangala ametembelea chumba cha upasuaji pamoja na chumba cha maabara na kuridhika na huduma zinazotolewa na kituo hicho na kuupongeza uongozi wa kituo hicho.
Wilaya ya Mbogwe ina jumla ya wakazi 215,404 lakini haina hospitali ya wilaya hivyo Mh Kigwangala ametoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kutilia mkazo ujenzi wa hospitali ya wilaya hata kwa kuanzia na jingo moja la wagonjwa wa nje
Vile vile Naibu waziri amesema zahanati zilizopo na vijiji havina uwiano kwani kwa wilaya nzima kuna zahanati 16 wakati vijiji vipo 86 hivyo kutoa maagizo kwa Mkurugenzi kuweka msisitizo kwenye ujenzi wa zahanati ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
Akitoa changamoto zinazoikabili idara ya afya Mganga Mkuu (W) Dr Erasto Ritte amemueleza naibu waziri kuwa wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu kwani jamii ya Mbogwe haitoi ushirikiano na hivyo kutegemea damu kutoka kwa wanafunzi tu
Pamoja na hayo ametoa changamoto ya watumishi pamoja na vitendea kazi , ikiwemo mashine ya Xray .
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.