KAMATI YA FEDHA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na miradi ya bara bara za Lugunga-Nhungiza yenye urefu wa km 13.0 , Mkweni-Nyankwiga-Nhomolwa yenye urefu wa km16.0 na KanegerePrison-Nhungiza yenye urefu wa km12.0. Miradi iliyokaguliwa hadi kukamilika itagharimu tsh104,000,000/=
Wakikagua miradi hiyo madiwani walilalamikia mitaro iliyowekwa kwenye barabara hizo kuwa imewekwa bila utaratibu unaoleweka na ipo chini ya kiwango, akijibu tuhuma hizo mhandisi wa ujenzi aliwaeleza madiwani kuwa mitaro hiyo ndio imeanza kufanyiwa kazi kwa hiyo wampe mkandarasi muda.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.