TAASIS ZA DINI ZAOMBWA KUTOA ELIMU YA LISHE
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe Furaha Chiwile amezitaka Taasis za Dini na asasi za kiraia kutoa elimu ya lishe ili kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto. Kaimu Mkurugenzi ameyasema hayo wakati wa kikao cha kamati ya lishe kilichokaa leo katika ukumbi wa Ngabanya Masumbwe.
Akiongea wakati wa kikao hicho Bi Chiwile amewaomba watumishi wa Mungu waliohudhuria kikao hicho kuhamasisha Elimu ya Lishe Makanisani na misikitini kwani hali ya watoto imekuwa mbaya hadi kupelekea watoto hao kutokufundishika mashuleni kwa sababu ya njaa.
Pamoja na hayo, Mratibu wa TASAF Mercy Joseph amesema kwa sasa miradi ya kutoa ajira za muda inayoongeza kipato kwa kaya masikini imejikita pia katika kilimo cha viazi lishe ,ambapo jumla ya eka 43 zimelimwa hivyo ni matumaini kuwa watoto pamoja na jamii nzima watapata chakula cha kutosha na kuongeza kipato kwakuwa vitauzwa na vingine vitatumiwa kama chakula.
Akiongea wakati wa kufunga kikao hicho bi Chiwile amewataka Waratibu wa lishe kuwashirikisha Maafisa Maendeleo yaJamii kwenye kata kwani wanauzoefu wa kuhamasisha hivyo itakuwa rahisi kutoa elimu ya lishe na wananchi kuwaelewa
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.