MKUU WA WILAYA YA MBOGWE AKAMATA MBAO 1889 NA MABANZI 570
Wananchi wa wilaya ya Mbogwe wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha kuwafichua wavunaji haramu wa mazao ya misitu. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe Martha Mkupasi alipofanya doria maalumu iliyoandaliwa na ofisi ya TFS kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) - Mbogwe kwa lengo la kukamata mazao ya misitu yaliyovunwa kinyume cha Sheria ya Misitu. Katika doria hii jumla ya mbao 1889 za vipimo tofauti tofauti na mabanzi 570 vilikamatwa kwenye kijiji cha Masumbwe, vitongoji vya Kibondo A na B.
Akiongea wakati wa zoezi hilo meneja wa TFS wilaya ya Mbogwe Yohana France aliwasisitiza wananchi wahakikishe wanazingatia taratibu za biashara ya mazao ya misitu ikiwa ni pamoja na kuwa na usajili, kulipa ushuru wa serikali na kuzingatia taratibu za uvunaji wa mazao ya misitu kama unavyoelekeza mwongozo wa uvunaji wa mazao ya misitu wa mwaka 2015, “Mazao yote yanayomilikiwa kinyume cha utaratibu ni haramu na yakikamatwa yatataifishwa na wamiliki kupewa adhabu kwa mujibu vifungu 88,89, 95 vya Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 na marekebisho yake”.
Pamoja na hayo Bwana Yohana aliwatahadharisha wananchi kujiepusha na matapeli wanaojiita watumishi wa Idara ya Maliasili na wanaopita mitaani kuwatapeli wananchi mali zao na kuwaomba rushwa kwa madai kuwa wametumwa na ofisi, tayari watu wawili ambao ni walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Summit iliyopo Masumbwe wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Akitoa taarifa fupi wakati wa zoezi la kusaka wavunaji haramu wa misitu, Meneja wa TFS (W) amemueleza Mkuu wa Wilaya kuwa wameshatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu taratibu za kuzingatia mtu anapotaka kufanya biashara ya mazao ya misitu na umuhimu wa kulinda rasilimali za misitu
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.