Agosti,2025 Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe. Sakina Mohamed amehitimisha ziara yake ya siku 3 kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa Wilayani kwa mwaka wa Fedha 2025/2026.
Miradi aliyotembelea leo ni pamoja na :-
1. Ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kabanga kata ya Nhomolwa yenye gharama ya TSH. 60,000,000
2. Ukamilishaji wa Zahanati ya Nyalubezi Kijiji cha Bukandwe Kata ya Bukandwe wenye gharama ya TSH. 24,000,000
3. Ukamilishaji wa Nyumba ya Watumishi 2 in 1 katika Kituo cha Afya Bukandwe kata ya Bukandwe wenye gharama ya TSH. 50,000,000
4. Eneo la Ujenzi wa Matundu 5 ya Vyoo na kichomea Taka katika Zahanati ya Kijiji cha Budoda Kata ya Masumbwe wenye gharama ya TSH. 40,459,438.01
5. Ukarabati wa Machinjio ya Masumbwe kata ya Masumbwe yenye gharama za TSH. 15,500,000
6. Ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Shenda Kata ya Masumbwe wenye gharama ya TSH. 24,000,000
7. Ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Busambilo Kata ya Iponya wenye gharama ya TSH. 24,000,000
8. Ujenzi wa Kichomea Taka katika Zahanati ya Lubeho kata ya Nyakafuru wenye gharama ya TSH. 21,000,000
Mhe. Sakina Mohamed ameendelea kusisitiza usimamizi mzuri wa miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kufunguliwa kwa wakati sahihi uliopangwa.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.