Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali, mstaafu Ezekiel E, Kyunga amewataka waaguzi kuwa na Moyo wa kujitolea na huruma kwa wagonjwa ,ameyasema hayo kwenye sherehe za siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika wilaya ya Mbogwe ,akiongea na wauguzi hao mkuu wa mkoa aliwakumbusha wauguzi juu ya umuhimu wao kwa wagonjwa
mkuu wa mkoa aliwaambia wauguzi wanadhamana kubwa juu ya maisha ya watu ,hivyo kuwataka kuwahudumia kwa upendo kwani kwa kufanya hivyo kutawapunguzia maumivu wagonjwa na kuwapa matumaini ya kupona.
wakisoma risala yao mbele ya mkuu wa mkuu wa mkoa wauguzi waliomba kulipwa malimbikizo yao wanayoidai serikali yakiwemo masaa ya ziada, malipo ya likizo, na malipo ya sare za kazi
wauguzi hao walisema licha ya waziri TAMISEMI Mh Simbachawene kutoa agizo la ulipwaji wa unifomu kwa wauguzi lakini bado hawajaanza kulipwa hela hizo na hivyo kuwafanya wauguzi kuvaa mavazi yaliyochakaa
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.