Madiwani wa halamshauri ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita,
wameshauriwa kufika kujionea miradi ya maendeleo badala ya kupokea
taarifa za watendaji wa kata ofisini.
Wito huo ulitolewa na Kaimu Mhandisi wa maji wilaya ya Mbogwe Suzana
Gogadi kwenye baraza la madiwani baada ya diwani wa kata ya Masumbwe
Shimo Kiyuyu kutoa taarifa ambayo siyo kweli kwa madai kuwa
miundombinu ya kutoa maji safi na salama nimibovu haitoi maji.
Gogadi alisema Miradi ya maji wa shenda – Masumbwe unavituo vya
kutolea maji (DP)20 na vyote vinafanyakazi na miundombinu yake ni
mizuri miongoni mwa vituo hivyo havitumiki kutokana na wananchi
kutumia maji ya visima vifupi.
Diwani wa kata ya Ushirika Daud Mabenga aliunga mkono hoja ya
mtaalamu na kuwaomba madiwani kuacha tabia ya kusubili taarifa za
maofisa watendaji wakata badala yake wafike kwenye miradi kujionea ili
wanapoletaa taarifa ziwe za kweli.
Awali Diwani wa kata ya Masumbwe Shimo Kiyuyu aliliambia baraza la
madiwani kuwa wakati mradi wa maji Shenda, masumbwe unaanza ulikuwa na
vituo 20 vya kutolea maji lakini kwa sasa ni vituo vinne tu ndiyo
vinafanyakazi vingine vibovu miundombinu yake.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mbobwe Sinzya Nsika alimwomba
Mkurugenzi kuwapatia semina Watendaji wa kata ili taarifa ziwe za
kweli na fupi aliwaomba madiwani kufika kujirizisha miradi ya
maendeleo ili kutoa vutana na wataalamu.
Nsika aliwaomba wataalamu kuwa na ushirikianao na madiwani ili
kuijenga wilaya ya Mbogwe hali ambayo italeta mabadiliko kuanzia ngazi
ya shina hadi wilaya na wananchi wajivunie serikali iliyopo madarakani
badala ya kukosa huduma.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.