"TUFANYE KAZI KWA BIDII NA WELEDI ILI KUIJENGA MBOGWE YETU."
Hayo yamesemwa leo 23 Oktoba,2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Adv. Edwin B. Lusa wakati akizungumza na Watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri mambo mbalimbali kwa maendeleo ya Mbogwe katika Ukumbi wa Mikutano uliopo jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.
Adv. Lusa amewaasa Watumishi wote kuzingatia kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu Yao sambamba na kufanya Kazi kwa Bidii na Weledi ili kuijenga Halmashauri yao.
Pia Lusa amewaasa Watumishi wote kushirikiana kikamilifu katika kusimamia Miradi ya Maendeleo inayoendelea Wilayani Mbogwe huku akiwasisitiza kuwa na Umoja,Mshikamano,Upendo na Nidhamu wakati wakitekeleza majukumu yao,vile vile kua na mshikamano katika ukusanyaji wa Mapato.
Aidha Adv. Lusa amewasisitiza Watumishi wote Kushiriki kwa wingi 29 Oktoba,2025 kupiga kura ili kupata Viongozi wazuri watakaosaidia kuleta Maendeleo.

Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.