17 Septemba,2025 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dr. Omari Sukari ameongoza kikao cha Waganga Wafawidhi,CHMT na RHMT kujadili Mada Mbali Mbali za kuimarisha Hudama za Afya katika Wilaya ya Mbogwe katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Masumbwe iliyopo kata ya Nyakafuru.
Mada zilizojadiliwa ni pamoja na :-
1. Mapato ya Vituo
2. Madeni ya Dawa
3. Matumizi ya Mfumo wa GOT-HoMiS
4. Kupulizia Dawa ya kuua vijidudu vya Malaria
5. Chanjo kwa Watoto
6. Mrejesho wa Usimamizi Shirikishi Ngazi ya Mkoa
Aidha Dr. Omari Sukari amesisitiza Vituo Vikusanye Fedha za kutosha ili kuwezesha uendeshaji wa vituo ikiwemo ununuzi wa Dawa na Vifaa Tiba pamoja na kulipa madeni ya Bohari ya Dawa (MSD)
Pia amewasisitiza Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea Huduma za Afya kuziba mianya ya upotevu wa mapato ikiwa ni pamoja na kufunga na kutumia mfumo wa GOT- HoMIS katika utoaji wa huduma za AFYA
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.