Kuelekea Kongamano kubwa litakalofanyika siku ya kupokea Mwenge wa Uhuru 2025,Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe leo tarehe 26 Agosti,2025 imefanya Kongamano lingine lililounganisha Vijana toka Tarafa ya Masumbwe yenye Kata za Lugunga,Nyajafuru,Masumbwe,Bukandwe,Nhomolwa na Iponya,Kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa Casablanca - Masumbwe na Mgeni Rasmi akiwa ni Mhe Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed,
Katika Kongamano hilo mada zilizotolewa ni pamoja na:-
1. Fursa za Kiuchumi kwa Vijana.
2. Uongozi
3. Uzalendo na Uadilifu
4. Afya na Afya ya uzazi kwa Vijana
5. Stadi za maisha na Stadi za Kazi
6. Malezi na Makuzi ya Vijana
7. Vijana kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.
Aidha Mhe. Sakina amewaasa Vijana kuzingatia Mafunzo waliyopewa kwani ni Mahususi kwao kujitambua, Uwajibikaji katika ujenzi wa taifa na kuwajengea uwezo Vijana kuhusu Fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.