08 Januari,2026 Kamati ya pembejeo Wilaya ya Mbogwe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mheshimiwa Sakina Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo imekutana kujadili mambo Mbalimbali ili kurahisisha upatikana wa Pembejeo kwa Wakulima.
Mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na:
1. Kuhakikisha Mkulima anauziwa Pembejeo zilizo na Ruzuku kupitia Mfumo wa Kidijitali.
2. Mamlaka zenye dhamana ziwasaidie wauzaji wa Pembejeo waliopo Vijijini kuweza kupata Uwakala wa Usambazaji wa Pembejeo zilizo na Ruzuku kupitia Mfumo.
3. Wakulima kuacha dhana Potofu juu ya zoezi la Upimaji Afya ya Udongo.
4. Kila Mkulima ahakikishe anajisajili ili kuweza kupata pembejeo za Ruzuku kupitia Mfumo pamoja na
5. Utoaji wa Elimu juu ya matumizi sahihi ya Pembejeo za Kilimo.
Kikao hiki kimekutanisha Wadau Mbalimbali wa Kilimo ikiwemo Mamlaka ya Kusimamia na Kudhibiti Ubora wa Mbolea(TFRA),Mamlaka ya Kusimamia na Kudhibiti Ubora wa Mbegu(TOSCI),Mamlaka ya Usimamizi wa Ubora wa Afya ya Mimea(TPHPA),Makapuni ya Mbolea,Wadau toka Benki Mbalimbali,Chama Kikuu cha Ushirika,Maafisa Ugani Kutoka Makao Makuu ya Halmashauri,Wa Kata na Vijiji pamoja na Wakulima Wawakilishi kutoka Kata Mbalimbali.
Kikao hiki kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi za Chama Kikuu cha Ushirika (Kagri) Kata ya Nyakafuru.


Picha za Wadau Mbalimbali walio hudhuria Kikao hicho

Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.