13 Mei,2025,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mhe. Vicent B. Lubaga ambae ni Mhe. Diwani wa Kata ya Nhomolwa ameongoza Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe kukagua Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa Wilayani Mbogwe kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na
1. Ujenzi wa Shule Mpya ya Amali iliyopo Kijiji cha Iboya Kata ya Mbogwe wenye Gharama ya TSH. 1,600,000,000/=, Fedha toka SEQUIP.
2. Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Msendamila Kata ya Ilolangulu wenye Gharama ya TSH. 80,213,494.21/=,Fedha toka SANITATION.
3. Ujenzi wa Nyumba ya Watumishi 2 in 1 katika Zahanati ya Kijiji cha Isebya Kata ya Isebya wenye Gharama ya TSH. 92,410,714.29/=, Fedha toka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) III kupitia Mradi wa TPRP IV(OPEC) Mwaka wa III wa Utekelezaji.
4. Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 4 na Matundu 6 ya Vyoo katika Shule ya Msingi Kagera Kata ya Ikunguigazi wenye Gharama za TSH. 113,600,000/=, Fedha toka BOOST.
5. Ujenzi wa Madarasa 2,Ukamilishaji wa Madarasa 6 na Ofisi 1 katika Shule ya Sekondari Lulembela wenye Gharama ya TSH. 125,000,000/=, Fedha toka Serikali Kuu
6. Ujenzi wa Mabweni 2 na Matundu 10 ya Vyoo katika Shule ya Sekondari Lulembela wenye Gharama ya TSH.281,000,000/=,Fedha toka SERIKALI KUU
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.