ISANJABADUGU WAMEKABIDHI VITENDEA KAZI KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mh Vicent Busiga.amepokea vinakilishi vitatu vyenye thamani ya Tsh 3,000,000 kutoka kwenye kikundi cha wachimbaji wadogo wadogo kinachoitwa Isanjabadugu kilichopo kwenye kata Nyakafulu wilayani Mbogwe.
Akiongea wakati wa makabidhiano, Mwenyekiti wa halmashauri amemshukuru Mungu kwa Neema ya machimbo mapya ya dhahabu yaliyogundulika hivi karibuni katika kata ya nyakafulu kwa kuwa ni neema ya pekee nakuwataka wachimbaji hao kusimamia vizuri eneo hilo na wahakikishe wanalipa kodi ya serikali kama inavyotakiwa,vilevile mwenyekiti amewataka waendelee kuihudumia jamii inayowazunguka na kuendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo ya wilaya hii kwani Wilaya bado ni changa na inakabiliwa na changamoto nyingi.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw Joseph Katemi Watwa, amesema wametoa msaada huo wa vinakilishi baada ya kutembelea ofisi za halmashauri na kugundua kuwa ofisi hizo zinakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendea kazi vikiwemo vinakilishi hivyo wakaamua kuchuka hatua ya kutoa msaada wa vifaa hivyo ili kupunguza changamoto hiyo. Bw Joseph ameendelea kusema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye shughuli zote za maendeleo ya wilaya pamoja na kulipa kodi zote za serika
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Elias Kayandabila ametoa shukrani kwa wachimbaji hao na kuwaomba waendelee kuunga mkono shughuli za maendeleo kwenye wilaya hii kwani wilaya bado ni changa na inakabiliwa na changamoto nyingi.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.