DC MBOGWE ATOA SIKU SABA KUPATA IDADI YA WATORO MASHULENI
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe, Martha Mkupasa ametoa siku saba kwa Maafisa Elimu kumuandalia ripoti ya utoro mashuleni, idadi ya watoto waliopata mimba wakiwa shuleni, pamoja na kubaini wazazi wote wanaosababisha watoto kutokufika shuleni.
Mkuu wa Wilaya ameyaongea hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na wananchi wa Tarafa za Lulembela na Mbogwe kilichofanyika jana kwenye Tarafa husika kikiwa na lengo la kuwakumbusha wazazi na walezi wajibu wao wa kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria shuleni pamoja na maswala ya ulinzi na usalama kwa ujumla.
Akitoa Elimu kwenye kikao hicho Afisa Elimu Msingi Samweli Muyemba amesoma waraka wa elimu no 2 wa mwaka 2001 unaohusu uandikishaji wa darasa la kwanza kwa watoto wenye umri wa miaka saba na waraka wa elimu no 6 wa mwaka 1998 unaohusu kumpa mimba mwanafunzi, kumuozesha mwanafunzi, kusimamia kuandikishwa,kuhudhuria na kuhitimu. Muyemba amesema amesoma waraka huo kwa wazazi ili watakapoanza kutoa adhabu kusiwe na malalamiko na ameahidi kusambaza waraka huo kwa walimu wakuu wote .
Wakati huo huo Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Goodluck Shayo ametoa elimu kuhusu uhamiaji haramu na kuwataka wananchi watoe ushirikiano wanapobaini kuhusu wahamiaji haramu kwani ni kosa la jinai kukaa, kumuajiri au kushirikiana na wahamiaji haramu hivyo wananchi watoe taarifa za wahamiaji hao kuepuka adhabu kwa mujibu wa sheria.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.