WATUMISHI WATAKAOSHINDWA KWENDA NA KASI YA AWAMU YA TANO WAKAE PEMBENI
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amewataka watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe kusimamima kikamilifu ukusanyaji wa mapato kwani mpaka sasa wamekusanya chini ya kiwango ,akizungumza na baraza la madiwani la robo ya tatu la mwaka wa fedha 2016/2017 lililofanyikia kwenye shule ya sekondari Masumbwe amewataka watendaji watakaoshindwa kwenda na kasi ya awamu ya tano kukaa pembeni.
Mkuu wa mkoa amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa bidii na kwa uweledi, na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo kuwaelimisha wananchi kuhifadhi chakula kutokana na hali ya ukame wananchi waelimishwe kutunza chakula.
Akiongea kwenye mkutano huo wa baraza la madiwani Katibu Tawala Mkoa wa Geita Selestine Gesimba amewataka watendaji wa halmashauri kuepuka kuzalisha hoja, na kuwataka wajibu hoja zote za wakaguzi hadi zifutwe. Vilevile katibu tawala aliwataka watu wa manunuzi kufanya kazi kwa uweledi na waache kufanya kazi kwa maslahi yao binafsi.
Akiongea wakati wa kufunga mkutano wa baraza mkuu wa wilaya ya Mbogwe Martha Mkupasi amewataka madiwani na watendaji kushirikiana kwenye swala la ukusanyaji wa mapato, madiwani wahamasishe wananchi kulipa kodi.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.