WANANCHI WALIOLIPIA CHF WAHUDUMIWE IPASAVYO.
MBUNGE wa Jimbo la Mbogwe Agustino Masele amemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Dr. Erasto Rite kuhakikisha anasimamia huduma za wananchi wake wote waliochangia huduma ya Afya CHF pindi wakifika kwenye Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya kutibiwa.
Mh Masele aliyasema hayo akiwa mgeni Rasmi katika hafla fupi ya kukabidhi gari la wagonjwa katika kituo cha afya cha Iboyo ambako alikabidhi gari hilo kwa niba ya Waziri wa Afya ,maendeleo ya jamii jinsia na watoto Ummy Mwalimu.
Kufuatia hatua hiyo Mh Masele alisema endapo wananchi hao wakihudumiwa ipasavyo watakuwa mabalozi wazuri wa kuwahamasisha wenzao kuchangia huduma hiyo ,na endapo wasipohudumiwa vyema wananchi hao watakuwa mabalozi wabaya sana na ndiyo watakuwa kikwazo kikubwa cha mafanikio ya mpango huo.
Sanjali na hilo amemtaka mganga huyo kukusanya michango hiyo ya Bima ya afya kwa wananchi hasa katika kipindi cha msimu wa mavuno ambapo kila mwananchi atakuwa na uwezo wa kuchangia bila bughudha.
Mganga mkuu wa wilaya hiyo Erasto Rite akatanabaisha kuwa wananchi wamepata elimu ya kutosha kuhusu kuchangia huduma hiyo ya CHF .
Dr Rite alitaja kuwa tangu mwaka 2016 mpaka januari 2017 jumla ya kaya 2370 sawa na asilimia 20% ya kaya 11475 wamejiunga na mfuko huo na wananafaidika na matunda hayo .
Aidha Dr Rite amemuahidi mbunge huyo kuwa atahakikisha anasimamia wataalamu wake wote waliochini yake kuhakikisha wanatoa huduma hiyo kwa weledi ili isije ikaleta shida .
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbogwe Elias Kayandabila baada ya kukabidhiwa ufunguo wa gari na kadi akamuahidi Mbuge Masele kuwa atahakikisha Gari hilo wanalitunza .
Akaipongeza Wizara ya Afya kwa kuwapatia Gari hilo ambalo mbunge amekuwa msaada mkubwa kwa ufuatiliaji kwani wananchi walitaabika sana kwani umbali wa kutoka vijiji vya Iboya, Ivumwa , Ilolangulu ni zaidi ya km 50.
Mwenyekiti wa kijiji cha Iboya masanja joseph kwa niaba ya wananchi wenzake ameishukuru serikali ya awamu ya Tano kwa kuitatua kero hiyo ya usafiri kwani wanawake wajawazito walipata shida wakati mwingine walijifungulia njiani wakiwa kwenye matera ya kukokotwa na Punda, Baiskeli hali iliyowapelekea kupoteza maisha.
Mwenyekiti huyo alisema serikali ya kijiji cha Iboya kata ya Mbogwe imetenga Hekta 28 za eneo la Hospitali ambalo serikali iweze kujenga Chuo ama shule ya wauguzi.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.