31 Julai,2025 Afisa Tarafa,Tarafa ya Mbogwe Bi Jacqueline Tairo amuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Bi. Sakina Mohamed katika Uzinduzi wa Kongamano la Vijana lililofanyika katika Kijiji cha Ushirika Kata ya Ushirika.
Katika Uzinduzi huo wa Kongamano vijana wameweza kujifunza yafuatayo:-
1. Fursa za Kiuchumi kwa Vijana.
2. Uongozi
3. Uzalendo na Uadilifu
4. Afya na Afya ya uzaazi kwa Vijana
5. Stadi za maisha na Stadi za Kazi
6. Malezi na Makuzi ya Vijana
7. Vijana kushiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.
Aidha Bi Jacqueline amewaasa Vijana kuzingatia Mafunzo waliyopewa kwani ni Mahususi kwa Vijana kujitambua, Uwajibikaji wa katika ujenzi wa taifa na kuwajengea uwezo Viana kuhusu Fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.