WANAKAMATI WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MBOGWE WAFUNDWA.
KWA muda mrefu kamati za shule za msingi zilikuwa zikiendesha shughuli zake bila ya kuelewa majukumu yao hali ambayo ilisababisha migogoro na migongano kati ya walimu na wanakamati hao.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi baada ya kubaini mapungufu hayo ikaamua kutenga fungu la uendeshaji wa mafunzo kwa wasimamizi wa shule yaani Kamati za shule ya kuwajengea uwezo.
Wilayani Mbogwe mkoani Geita wameendesha mafunzo ya wiki mbili akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Afisa Elimu msingi Samwel Muyemba amesema jumla ya washiriki 1027 toka shule za msingi 84 kwa kata 19walipata mafunzao ya kuwajengea uwezo wa uendeshaji wa majukumu ya kamati za shule.
Mwl Muyemba amesema mfunzo hayo yaliendeshwa kwa muda wa wiki mbili katika vituo saba(07)vya shule za sekondari za masumbwe ,Nyakafuru,Ilolangulu, Lugunga na katika shule za msingi za Lulembela,Itimbya na Isangijo.
Afisa huyo amesema Mada mbalimbali zilitolewa kwa washiriki ambazo ni Uongozi,Muundo wa majukumu ya Kamati za shule,usimamizi wa Sera na sheria za uendeshaji wa Elimu,usimamizi wa Raslimali za shule,uendeshaji wa mpango wa maendeleo ya shule
Amesema mahudhulio yalikuwa mazuri kwa washiriki ambapo asilimia 99%walihudhulia mafunzo pia mitihani mablimbali ilitolewakwa washiriki.
Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wenyeviti wa kamati na wanakamati za shule wameipongeza serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuwapatia mafunzo hayo.
Wamesema baada ya kupatiwa mafunzo hayo wameeiva na wanamuahidi kuwa watazisimamia shule kwa weledi na pia wametambua kuwa shule hizo ni mali yao wananchi ,ila wameomba mafunzo hayo yawe kila mwaka kwa kukumbushana majukumu .
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.