WANANCHI WA WILAYA YA MBOGWE WALALAMIKIA NGURUWE PORI
Wananchi wa kata ya Bukandwe Wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita wako hatarini kukumbwa na Baa la njaa endapo serikali haitachukua hatua za maksudi kukabiliana na Nguruwe Pori ambao wamekuwa wakivamia na kula mazazo ya chakula kama vile mihogo ,viazi na mahindi mashambani mwao.
Diwani wa kata ya Bukandwe Joseph Kilonja ametoa malalamiko yake kwenye baraza la madiwani la awali akiwasilisha hali ya usalama wa kata hiyo. Kilonja ameilalamikia serikalini kutokuchukua hatua dhidi ya wanyama hawa waharibifu wa mazao.
Akiunga mkono na kuitetea hoja hiyo diwani wa kata ya Ushirika Daudi Mabenga anasema swala la nguruwe pori kwenye kata ya Bukandwe limekuwa tatizo la muda mrefu ameiomba serikali kuingilia kati swala hilo ili kuiokoa jamii na baa la njaa
Akijibu hoja hiyo kwa madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji afisa Mifugo wilaya hiyo Nicholaus Ngulinzila alisema tatizo la nguruwe pori linafahamika na tayari wameshaanza kuchukua hatua muhimu za kumaliza kabisa tatizo hilo
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.