Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe. Sakina Mohamed ametembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa Wilayani Mbogwe.
Miradi aliyotekelezwa ni pamoja na:-
1. Ukamilishaji wa Zahanati ya kijiji cha Nambubi Kata ya Mbogwe wenye gharama ya TSH. 24,000,000.00
2. Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa katika Shule ya Msingi Isebya Kata ya Isebya wenye gharama ya TSH. 25,000,000.00
3. Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo vya Elimu ya Awali katika Shule ya Msingi Nyashinge Kata ya Isebya wenye gharama ya TSH. 70,100,000.00
4. Ukamiloshaji wa Jengo la OPD katika Kituo cha Afya Ikunguigazi Kata ya Ikunguigazi wenye gharama ya TSH. 50,000,000.00
5. Ujenzi wa Vyumba 4 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo katika Shule ya Msingi Majengo Kata ya Lulembela wenye gharama ya TSH. 113,600,000.00
6. Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo Vya Elimu ya Awali katika Shule ya Msingi Mtakuja Kata ya Lulembela wenye gharama ya TSH. 132,700,000.00
7. Ukamilishaji wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Lulembela Kata ya Lulembela wenye gharama ya TSH. 16,846,550.00
8. Ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kashelo Kata ya Lulembela.
Aidha Mhe. Sakina amewaasa wasimamizi wa miradi hiyo waweze kusimamia kwa weredi na ukamini ili miradi hiyo iweze kumalizika kwa wakati na kufunguliwa kwa ajili ya natumizi yanayotakiwa
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.