13 Agosti,2025 Ikiwa ni siku ya 2 katika Muendelezo wa Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe. Sakina Mohamed,ameendelea kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa Wilayani Mbogwe kwa mwaka wa Fedha 2025/2026.
Miradi aliyoitembelea na kukagua ni pamoja na:-
1. Uchimbaji wa kisima Kirefu na Ujenzi wa Matundu 5 ya Vyoo katika Kituo cha Afya Kakumbi Kata ya Lugunga wenye gharama ya TSH. 68,582,409.91
2. Ukamilishaji wa Vyumba 3 vya Madarasa,Ujenzi wa Chumba 1 cha Darasa na Ujenzi wa Matundu 5 ya Vyoo Elimu Msingi na Eneo la Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Ujenzi wa Matundu 3 ya Vyoo Shule ya Awali katika Shule ya Msingi Mapinduzi iliyopo Kata ya Lugunga wenye gharama ya TSH. 133,700,000.00
3. Eneo la Ujenzi wa Shule Mpya ya Elimu ya Awali katika Shule ya Msingi Lugunga wenye gharama ya TSH. 330,700,000.00
4. Ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Mponda Kata ya Lugunga wenye gharama ya TSH. 24,000,000.00
5. Eneo la Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 12 ya Vyoo Elimu Msingi na Eneo la Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo Elimu ya Awali katika Shule ya Msingi Bulilila Kata ya Nyasato wenye gharama ya TSH. 145,300,000.00
6. Eneo la Ujenzi wa vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo Elimu ya Awali katika Shule ya Msingi Mlale Kata ya Ushirika wenye gharama ya TSH. 70,100,000.00
7. Ukamilishaji wa Darasa 1 katika Shule ya Msingi Ushetu Kata ya Ushirika wenye gharama ya TSH. 12,5000,000.00
8. Eneo la Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo Elimu Ya Awali katika Shule ya Msingi Kadoke kata ya Ushirika wenye gharama ya TSH. 70,100,000.00
9. Ukamilishaji wa Ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Bunigonzi kata ya Bunigonzi wenye gharama ya TSH. 40,000,000.00
10. Eneo la Ujenzi wa vyumba 3 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo katika Shule ya Msingi Mwabukwalule kata ya Bunigonzi wene gharama ya TSH. 88,600,00.00
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.