Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel Robert amewataka wananchi kushiriki katika maendeleo ya Wilaya zao kwani maendeleo yataletwa na wananchi wenyewe na hakuna mtu kutoka nje atakuja kuwaletea maendeleo.
Mhandisi Robart ameyamesema hayo alipofanya ziara ya kikazi Wilayani Mbogwe, Kata ya Ikobe kijiji cha Kagongo, baada ya wananchi hao kutokuwa na Zahanati wala shule ya msingi hivyo kupelekea watoto kufuata elimu mbali na wengine kutokwenda shule. Katika Kijiji hicho Mkuu wa Mkoa aliendesha harambee ya ununuzi wa kiwanja cha kujenga Zahanati jumla ya milioni moja ilipatikana ambapo laki tano itatumika kununua kiwanja na laki tano zitaanza ujenzi wa zahanati hiyo.
Akiwa katika ziara yake Mkuu wa Mkoa alishiriki kwenye zoezi la kuchimba msingi wa Zahanati ya Kijiji cha Msendamila, pia alitoa maagizo kuwa ndani ya wiki mbili Vijiji vyote vya Mkoa wa Geita viwe vimemamaliza kuchimba msingi ya Zahanati.
Pamoja na hayo mkuu wa wilaya ya Mbogwe Mhe. Martha Mkupasi amewataka wananchi wa Kata ya Iponya kujshirikiana na kuleta maendeleo kwani maendeleo hayana vyama wala ukabila, Mkupasi ameyasema hayo wakati wa kuzindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha bunyihuna. Kata ya Iponya ina jumla ya vijiji 6 na ina Zahanati moja tu ambayo inahudumia wananchi wa Kata nzima.
Wananchi wa Iponya wamempongeza Mkuu wa Wilaya kwa Juhudi anazofanya za kuleta maendeleo ya Wilaya ya Mbogwe, wananchi hao wamesema hawajawahi kutembelewa na Mkuu wa Wilaya tangu kuanzishwa kwa kata hiyo, huvyo wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwakumbuka.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.