MBOGWE WAAZIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI KWENYE GEREZA LA KANEGERE.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe wameazimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti kwenye eneo la Gereza la Kanegere . Akiongea baada ya kupanda miti Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) ,Bi Furaha Chiwile amewataka wananchi na watumishi kwa ujumla kupanda miti kwa wingi na kuitunza na waepuke kukata miti ovyo kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha mazingira na vyanzo vya maji.
Jumla ya miti 200 ilipandwa lengo likiwa ni kupanda miche 2500 kwenye eneo hilo la magereza. Miche hiyo inayofadhiliwa na TASAF awamu ya tatu inapandwa kwenye Taasisi za serikali wilayani Mbogwe.
wakati huo huo Afisa Mazingira wa Wilaya Charles Karibu Tuyi alisema “ Kauli Mbiu ya Siku ya Mazingira kitaifa ni Hifadhi Mazingira Mhimili kwa Tanzania ya Viwanda”. Amewashukuru watu wote waliojitokeza kupanda miti na amewaomba waonyeshe ushirikiano wa kuitunza miti hiyo kwani itasaidia sana kutunza vyanzo vya maji .
Pamoja na hayo ,Afisa Mazingira (W) alikabidhi jumla ya miche 920 kwa mwakilishi wa mkuu wa Gereza Sgt. Kuyi Kalulumila ambaye ameahidi kuitunza miche hiyo na amemshukuru Mkurugenzi kwa kulikumbuka gereza hilo kwani lina eneo kubwa na linauwezo wa kutunza miti hiyo.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.