Madiwani Mbogwe Wapitisha Bajeti kwa Mwaka 2018/2019
Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Limejadili na kuridhia kupitisha rasimu ya bajeti yenye zaidi ya shilingi 31,292,669,600/= ikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa Fedha 2018/2019 ambapo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ni bilioni 1,377,965,900 kati ya fedha zote .
Akiwasilisha rasimu ya bajeti kwenye kikao maalum cha Baraza, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Bw Daud Lucas ,amesema Halmashauri inatarajia kukusanya , kupokea na kutumia zaidi ya Bilioni 31.292,669,600 ambapo kati ya fedha hizo Bilioni 10.988 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, 762,288,000 ni ruzuku kutoka serikali kuu(OC) 18.141 ni mishahara ya watumishi na bilioni 1.377 ni makusanyo ya ndani
Lucas amevitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kuwa inaangazia ukamilishaji wa miradi ambayo haikukamilika kwa miaka ya nyuma hususani ukamilishaji wa Miradi ya Afya na Elimu, ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kieletroniki ,kutoa huduma bora za kijamii, pamoja na kuinua uchumi wa wananchi
“Mhe Mwenyekiti rasimu hii ya mpango wa bajeti ya Halmashauri ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019, na itaendelea kujadiliwa na kupatiwa ushauri kwenye vikao vya ngazi ya Mkoa, ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango kabla ya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge” alibainisha Bw Lucas
Akiongea wakati wa kufunga kiako hicho,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mhe Vicent Busiga Amewataka Madiwani kutoa Ushirikiano kwenye zoezi la ukusanyaji mapato pamoja na kubuni vyanzo vyanzo vipya vya mapato ili yasaidie kuharakisha maendeleo.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.