21 JULAI,2025 MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE Adv. EDWIN B. LUSA AMEONGOZA WAJUMBE WA KAMATI YA MENEJIMENTI YA WILAYA (CMT) KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO INAYOENDELEA KUTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na:-
1. Ujenzi wa Mabweni Mawili,Vyumba Viwili vya Madarasa na Matundu Kumi ya Vyoo katika Shule ya Sekondari Masumbwe Kata ya Nyakafuru wenye jumla ya TSH. 331,000,000/= ,Ujenzi umekamilika kwa Asilimia 94.
2. Ujenzi wa Mabweni Mawili,Vyumba Viwili vya Madarasa na Matundu Kumi ya Vyoo Katika Shule ya Sekondari Nyakasaluma Kata ya Masumbwe wenye jumla ya TSH. 331,000,000/= Fedha toka SEQUIP,Ujenzi umekamilika kwa Asilimia 94.
3. Ujenzi wa Jengo la OPD kwenye Kituo cha Afya Nyakafuru kata ya Nyakafuru wenye Gharama ya TSH. 100,000,000/= fedha toka Mapato ya Ndani,Ujenzi hatua ya Ukamilishaji.
4. Ujenzi wa Vyumba Viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Nyasato Kata ya Nyasato wenye gharama ya TSH. 35,000,000/= Fedha toka Serikali Kuu,Ujenzi umekamilika kwa Asilimia 96.
5. Ujenzi wa Shule Mpya ya Amali wenye gharama ya TSH. 1,600,000,000/= Fedha toka Serikali Kuu,Ujenzi upo hatua ya Ukamilishaji.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.