Ni wapi Huduma Zinazohusu Miundombinu ya Barabara na Majengo zinapatikana?
Wananchi wote mnakaribishwa kupata ushauri na maelekezo bure juu ya huduma za miundombinu ya barabara na majengo, huduma hii inapatikana katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kupitia Ofisi ya Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya ya Mbogwe.
Aidha wananchi wanapaswa kulinda, kutunza na kuwa na matumizi sahihi ya miundombinu ya barabara na majengo iliyokwishaanza kutumika.