• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Frequently Asked Questions |
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe

The United Republic of Tanzania MBOGWE DISTRICT COUNCIL MBOGWE DISTRICT COUNCIL

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Administration and human resource
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Finance and Business
      • Social Work
      • Health
      • Ardhi na Mali Asili
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji na Udhibiti Majitaka
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
    • Units
      • Procurement and Supply
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa na Uwekezaji
  • Huduma
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Hamashauri ya Mbogwe
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya Na Maji
      • Kamati ya Maaadili
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Bodi ya Ajira
      • Alat Mkoa
      • Kamati ya Vileo
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi(CMAC)
      • Kamati ya Kugawa Ardhi
      • Kamati ya LAVULAK
  • Miradi
    • Project Projection
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha za Matukio mbalimbali
  • Machapisho
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu mbalimbali

Waziri Mkuu Ataja Mikoa Minne Inayoongza kwa Utoro Shuleni

Posted on: April 1st, 2018

WAZIRI MKUU ATAJA MIKOA MINNE INAYOONGOZA KWA UTORO WA WANAFUNZI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaja mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa sekondari.


Waziri mkuu pia ameitaja mikoa ya Rukwa, Geita, Tabora, Singida na Simiyu kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi.


Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa ameitaja mikoa hiyo leo Jumatatu Aprili 2,2018 akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Magogo mkoani Geita.

Mbio za Mwenge zitakazohitimishwa Oktoba 14,2018 mkoani Tanga zinaongozwa na kauli mbiu “Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya nchi yetu.”


Majaliwa amesema Mkoa wa Tabora unaongoza kwa asilimia 9.7 ya wanafunzi watoro wa sekondari ukifuatiwa na Geita (asilimia 8.1), Mtwara (asilimia 6.1) na Shinyanga (asilimia 6.3).

Kwa shule za msingi, Rukwa inaongoza kwa asilimia 3.2, ukifuata Geita (asilimia 3.1), Tabora (asilimia 2.9), Singida (asilimia 2) na Simiyu (asilimia 2).


“Kwa jumla utoro wa wanafunzi wa sekondari ni mkubwa kuliko shule za msingi. Naikumbusha mikoa yote niliyoitaja kuhamasisha wananchi wakiwamo wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni kwa kutumia utaratibu wa sheria zilizowekwa,” amesema Majaliwa.


Aidha , Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mheshimiwa Jensita Mhagama ameelezea kuwa mwenge ni Chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa ,Mwl Julius Kambarage Nyerere Mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika.


“Mbio za mwenge wa uhuru zilianza rasmi mwaka 1964 baada ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliozaa nchi inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”Alisema Waziri Jenista.


Mwenge wa uhuru utakimbizwa katika mikoa yote 31 ya Tanzania katika halmashauri 195 na kwa muda wa siku 195.


Sherehe hizo zilizosindikizwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili, kwaya, na halaiki zilifana na zimehudhuria na wakazi wengi.


kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru ni” Elimu ni ufunguo wa maisha ,wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa”

Announcements

  • Watoto wa kike waliokatisha Masomo yao November 01, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA USAJILI WA ANWANI ZA MAKAZI March 09, 2022
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi kwa Walimu September 06, 2020
  • Ratiba ya Kampeni za Kampeni Jimbo la Mbogwe August 26, 2020
  • View All

Latest News

  • WAENDESHA VIFAA VYA BIOMETRIKI NA WAANDISHI WASAIDIZI WAKIPATA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • MAFUNZO YA WAENDESHA VIFAA VYA BIOMETRIKI NA MAFUNZO YA WAANDISHI WASAIDIZI YAMEFANYIKA LEO TAREHE 29 APRILI,2025

    April 29, 2025
  • TAARIFA YA MKAGUZI WA MAHESABU

    June 26, 2024
  • Progamu ya utoaji wa Chakula Mashuleni wilayani Mbogwe

    May 20, 2022
  • View All

Video

UFUNGUZI WA MAJENGO MAPYA NA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA CHA MASUMBWE, GEITA
More Videos

Quick Links

  • MKOA WA GEITA
  • WIZARA YA TAMISEMI
  • IKULU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  • MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA)
  • BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA(NECTA)
  • WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
  • WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TKNOLOJIA
  • WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Related Links

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora
  • Mkoa wa Geita

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita

    Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe

    Telephone: +255734412592

    Mobile: +255734412592

    Email: ded@mbogwedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.