WATU WATATU WAJERUHIWA KWENYE TETEMEKO LA ARDHI WILAYANI MBOGWE
Wananchi watatu wa kijiji cha Bwendamwizo kata ya Ngemo wilayani Mbogwe wamepata majeraha pamoja nanyumba nne kubomoka kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea usiku wa kuamkia jumapili.
Tetemeko hilo limesababisha uharibu mkubwa kwenye Taasisi za umma zikiwemo shule zahanati na kituo cha kilimo. Maeneo yaliyoathirika kwa kiwango kikubwa ni kata za Ngemo na Ushirika ambapo shule ya sekondari Isangijo madarasa na maabara pamoja na hosteli za wanafunzi vimepata nyufa na nyumba za waalimu zimedondoka.Katika kata hiyo hiyo ya ushirika zahanati pamoja na kituo cha kilimo vimepata nyufa .
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe Martha Mkupasi amewatembelea wahanga na kuwapa pole waathirika wa tetemeko hilo na kuwataka wananchi kujenga nyumba imara ili kupunguza madhara yanayoweza kutokea kipindi cha majanga, aidha amemuagiza Mhandisi wa Ujenzi kufanya tathimini ya uharibu wa majengo ya umma na kumpa taarif
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.