WATAALAMU WA AFYA YA WANYAMA WAKISHIRIKIANA NA WATAALAMU WA AFYA YA BINADAMU WAMETOA ELIMU KWENYE SHULE ZA MSINGI KUHUSU ELIMU JUU YA UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA.
Katika kuadhimisha Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani tarehe 28/07/2025, Wataalamu toka Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe wamefanya maadhimisho haya mapema siku ya Ijumaa tarehe 26/09/2025
Ikiwa ni lengo la kuwapa Elimu wanafunzi kuhusu Ugongwa huu hatari wa Kichaa cha Mbwa
Timu ya wataalamu ilitembelea shule sita za Tarafa ya Masumbwe zilizopo katika kata mbili za Nyakafuru na Masumbwe ambazo ni: Shule za Msingi Uhuru, Muungano, Masumbwe, Mkapa, Loen na Johnson.
Kati ya hizo, shule 2 ni Shule binafsi na 5 ni za Serikali, ambapo jumla ya wanafunzi waliohudhuria Mafunzo hayo na kupata Elimu ni zaidi ya Wanafunzi 3,600.
Elimu zilizotolewa ni pamoja na:-
1. Ufafanuzi wa ugonjwa wa kichaa cha mbwa– ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi na huathiri mifumo ya fahamu ya wanyama na binadamu.
2. Njia za maambukizi– huambukizwa hasa kupitia kuumwa na mbwa mwenye ugonjwa au mnyama aliyeambukizwa kama paka, punda n.k.
3. Kinga kwa wanyama – kuchanja mbwa na paka mara kwa mara.
4. Jinsi ya kujikinga na ugonjwa. kuepuka kusogelea, kushika au kuchokoza mbwa usiowajua kwa kupiga mawe au fimbo au kupiganisha / kushindanisha mbwa.
5. Kama mtu amengatwa: osha kidonda kwa maji na sabuni kwa dk 15, Toa taarifa mara moja kwa mzazi / mtu mzima unayeishi nae. Hakikisha mnafika hospitali ya serikali kwa ajili ya kupata kinga dhidi ya ugonjwa huu.
6. Hakuna tiba kwa binadamu au mnyama ambaye anaonesha dalili za ugonjwa.
5. Hatua za kujikinga – kuhakikisha mbwa wote wa kufugwa wanachanjwa, kutoacha mbwa kuzurura mitaani, na kutoa taarifa kuhusu mbwa wakali au wazururaji.
Kwa ujumla, zoezi hili limeongeza uelewa kwa wanafunzi na kuchochea hamasa ya jamii katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha Mbwa na Jinsi ya Kujikinga.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.