Wasimamizi wa Vituo na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupiga Kura wameanza Mafunzo.
26 Oktoba,2025 Wasimamizi Wa Vituo na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupiga Kura kwa Tarafa ya Masumbwe wameanza Mafunzo ya Siku mbili katika Ukumbi wa Subira uliopo Mzambarauni Kata ya Nyakafuru,ikiwa ni Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika siku ya Junatano Oktoba 29,2025.
Akifungua Mafunzo hayo Msimamizi Msaidizi Ngazi ya Jimbo Jimbo la Mbogwe Bi. Sarah Membo kwa Niaba ya Msimamizi Wa Uchaguzi Jimbo la Mbogwe Ndg, Ng'ambu Manyonyi amewaasa wasimamizi hao kufuata Sheria na Taratibu zote za Uchaguzi kwa Kipindi chote cha Uchaguzi.
Mafunzo haya yamegawanyika katika Tarafa zote 3 ambapo Tarafa ya Masumbwe wanafanya Mafunzo katika Ukumbi wa Subira uliopo Kata ya Nyakafuru,Tarafa ya Mbogwe wanafanya Mafunzo katika Bwalo la Shule ya Sekondari Mbogwe kata ya Mbogwe na Tarafa ya Ilolangulu wanafanya Mafunzo katika Ukumbi wa Masasi Uliopo Lukembela kata Ya Lulembeka.


Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.