Mkoa wa Geita unatarajia kuanza zoezi la chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa Wasichana wenye Umri wa miaka kumi na nne(14) lengo likiwa ni kuwakinga na maambukizi ya virusi vya human papilloma.
Saratani ya Mlango wa kizazi imekuwa ikiongezeka kila mwaka kwa nchi na takribani watu elfu hamsini wamekuwa wakiongezeka na kusababisha vifo vya wakina mama wengi pamojana na mabinti.
Akizungumza na wadau wa sekta ya afya Mkoani Humo,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel ametaja sababu ambazo zimeendelea kusababisha saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kujamiiana kwenye umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi ndoa za mitaara pamoja na uvutaji wa sigara.
“Ndugu washiriki baadhi ya dalili za ugonjwa wa saratani ni pamoja na Kutokwa kwa damu bila mpangilio au kutokwa damu baada ya kujamiana Maumivu ya mgongo, miguu au kiuno Kuchoka, kupungua uzito, kupungikiwa hamu ya kula Kutokwa uchafu uchafu kwenye uke uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu Kuvimba mguu mmoja”Alisema Robert.
Kwa upande wake Mratibu msaidizi wa Afya ya uzazi Mkoani humo,Bi Mbeleje Dornad alisema kwa hapa nchini takribani wanawake laki nne na sitini na tisa elfu wamegundulika na maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi.
“Inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi, na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea”Alisema Bi,Mbeleje.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita,Joseph Odero amewataka wazazi pamoja na walezi kutoa ushirikiano pindi zoezi hilo litakapo anza tarehe 23 mwezi huu wa aprili ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu mabinti wenye umri wa miaka 14 kufanyiwa chanjo hiyo.
Takwimu kutoka hospitali ya Occean Road inaonyesha kwamba, Saratani ya Mlango wa Kizazi inachangia kwa asimilia 36 ya saratani zote, Asilimia 70 ya wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi wanajitokeza katika hatua ambayo tayari saratani imesha samba maeneo mengine mwilini.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.