• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Frequently Asked Questions |
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe

The United Republic of Tanzania MBOGWE DISTRICT COUNCIL MBOGWE DISTRICT COUNCIL

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Administration and human resource
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Finance and Business
      • Social Work
      • Health
      • Ardhi na Mali Asili
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji na Udhibiti Majitaka
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
    • Units
      • Procurement and Supply
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa na Uwekezaji
  • Huduma
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Hamashauri ya Mbogwe
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya Na Maji
      • Kamati ya Maaadili
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Bodi ya Ajira
      • Alat Mkoa
      • Kamati ya Vileo
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi(CMAC)
      • Kamati ya Kugawa Ardhi
      • Kamati ya LAVULAK
  • Miradi
    • Project Projection
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha za Matukio mbalimbali
  • Machapisho
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu mbalimbali

Wananchi wa Kata ya Iponya Wapokea kwa Kishindo zoezi l Usajili wa vyeti vya Kuzliwa kwa watoto wenye Umri Chini ya Miaka Mitano

Posted on: May 16th, 2017

WANANCHI  WA  KATA  YA  IPONYA  WILAYANI  MBOGWE, GEITA WAPOKEA KWA  KISHINDO  ZOEZI  LA  USAJILI  WA VYETI  VYA KUZALIWA  KWA  WATOTO  WENYE  UMRI  CHINI  YA  MIAKA MITANO

Kata ya Iponya  imevuka lengo la uandikishaji watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa ajili ya kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kwa zaidi ya watoto 900 sawa na 154.7%

Kauli hiyo ilitolewa na mratibu wa zoezi la usajili wa  watoto chini ya umri wa miaka mitano wa wilaya ya Mbogwe bwana  Fredrick Chotamasege,  alipokuwa akiwasilisha taarifa ya hali ya uandikishaji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe aliyefanya ziara ya ufuatiliaji katika kata ya Iponya.

“Kata ya Iponya imefanikiwa kuvuka lengo katika zoezi la uandikishaji watoto chini ya umri wa miaka mitano  zoezi  linaoendeshwa na wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). Kata ya Iponya iliwekewa lengo la kuandikisha watoto 1,806 lakini hadi  kufikia   tarehe 16/05/2017 ilikuwa imeandikisha watoto 2,794” alisema Fredrick. Aliongeza kuwa usajili huo ni sawa na ongezeko la watoto 988 waliosajiliwa sawa na  54.7%.

Pamoja na mafanikio makubwa ya  zoezi  hilo,zipo  changamoto za mawasiliano ya  mtandao wa Tigo  unaotumika kutuma  takwimu hizo.  Aliongeza  kuwa mtandao huo umekuwa ukitumia muda mrefu kutuma majina na hivyo kusababisha kuwa na takwimu tofauti kati ya zile zilizopo kwenye vitabu na zile za kwenye mtandao wa RITA.

Haya yalielezwa wakati  Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Elias Kayandabila, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya zoezi la uandikishaji watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika kata za Masumbwe na Iponya wilayani Mbogwe.

Hata hivyo, baada ya Mkurugenzi Bw. Kayandabila kuridhika na hatua za uandikishaji aliwaagiza waratibu wa zoezi hilo kwenye kata kufanya ukaguzi wa vitabu (physical verification) ili kupata takwimu halisi kama alivyoshiriki yeye mwenyewe kwenye kata ya Iponya na Masumbwe ,ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tatizo la kimtandao.

Bw.Kayandabila alisisitiza kuwa “  Mbogwe ni miongoni mwa wilaya zenye mwingiliano wa watu na  nchi  jirani, hivyo amewaagiza waratibu wa zoezi  kuorodhesha watoto wote ambao wanakuja bila kadi ya kliniki au tangazo la kuzaliwa ili waweze kufuatiliwa na kujiridhisha kama kweli wamezaliwa hapa nchini licha ya kupata barua za utambulisho kutoka serikali ya kijiji.

Mkurugenzi amewasihi wazazi wa  watoto kuwa na makubaliano ya majina kabla hawajaenda kwenye vituo vya kusajilia ili kupunguza changamoto iliyojitokeza kwa baadhi ya wazazi kutoelewana juu ya  majina ya watoto na hivyo kusababisha kuharibika kwa vyeti .



Announcements

  • Watoto wa kike waliokatisha Masomo yao November 01, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA USAJILI WA ANWANI ZA MAKAZI March 09, 2022
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi kwa Walimu September 06, 2020
  • Ratiba ya Kampeni za Kampeni Jimbo la Mbogwe August 26, 2020
  • View All

Latest News

  • WAENDESHA VIFAA VYA BIOMETRIKI NA WAANDISHI WASAIDIZI WAKIPATA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • MAFUNZO YA WAENDESHA VIFAA VYA BIOMETRIKI NA MAFUNZO YA WAANDISHI WASAIDIZI YAMEFANYIKA LEO TAREHE 29 APRILI,2025

    April 29, 2025
  • TAARIFA YA MKAGUZI WA MAHESABU

    June 26, 2024
  • Progamu ya utoaji wa Chakula Mashuleni wilayani Mbogwe

    May 20, 2022
  • View All

Video

UFUNGUZI WA MAJENGO MAPYA NA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA CHA MASUMBWE, GEITA
More Videos

Quick Links

  • MKOA WA GEITA
  • WIZARA YA TAMISEMI
  • IKULU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  • MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA)
  • BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA(NECTA)
  • WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
  • WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TKNOLOJIA
  • WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Related Links

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora
  • Mkoa wa Geita

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita

    Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe

    Telephone: +255734412592

    Mobile: +255734412592

    Email: ded@mbogwedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.