BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe limeridhia kuomba Shirika la TANESCO kupeleka Umeme wa REA katika maeneo ya Migodi ili gharama za uendeshaji kwa wananchi ziweze kupungua.
Awali akiwasilisha ombi hilo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Elias Kayandabila amesema Mbogwe imejaliwa kuwa na fursa nyingi za uchimbaji mdogo wa Madini ya Dhahabu , ambapo uchimbaji huo unapelekea wananchi kuongeza kipato na kuinua hali ya kiuchumi ya familia zao pia unaongeza mapato ya Halmashauri.
Kayandabila amesema kuwa ni maeneo mengi umeme huo wa REA mpaka sasa haujafika na hivyo kupelekea gharama za uendeshaji wa shughuli za uchimbaji kuwa kubwa kwa sababu ya mitambo ya kuchimba dhahabu inategemea raslimali ya mafuta hivyo gharama kuwa kubwa na faida baada ya uzalishaji kupungua .
Mkurugenzi huyo ameyataja maeneo ya ambayo hayajafikiwa na umeme wa REA na ndiyo yaliyo na fursa hiyo ya dhahabu ardhini ni Nyakafulu,Bulanga ,Kakumbi Mpya chini ya Shule ,kanegere na Bukandwe.
Wilaya ya Mbogwe ni miongoni mwa Wilaya ambazo zimefanikiwa kupitiwa na umeme wa Rea Katika Mkoa wa Geita mradi ambao unasimamiwa na Shirika la Tanesco chini ya Mkandarasi ELTEL kwa ufadhili wa Banki ya maendeleo ya Afrika (ADB)Na inatarajia hadi kukamilika mradi utanufaisha vijiji vyote 86 vya wilaya ya Mbogwe.
Kwa upande wake meneja wa Tanesco Wilaya ya Mbogwe Weston Njejo amesema kuwa wao watapokea maombi ambayo wameainisha maeneo na wao watayafikisha REA.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.