Idara ya uhamiaji Mkoani Geita imewakamata Raia wa Burundi Thelathini (30) ambao wanaishi na kufanya kazi Nchini kinyume cha sheria na wengine wakikamatwa kwenye zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya Taifa ambalo linaendelea Mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za uhamiaji Mkoani humo,Naibu kamishina wa idara ya uhamiaji Mkoani Geita, Wilfred Marwa amesema kati ya hao Raia kumi na nane ( 18) ambao wapo nchini kinyume na sheria na wanafanya kazi mbalimbali za kujiingizia kipato na wengine kumi na mbili (12) walikuwa kwenye zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya Taifa jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Naibu kamishina Marwa ametaja kazi ambazo wamekuwa wakizifanya Raia hao wa kigeni kuwa ni kazi za kilimo na ufugaji.
“Mara nyingi watu hawa wanajishughulisha sanaa na kazi za ufugaji wa Ng’ombe na kilimo cha
Mananasi pamba na mpunga kwenye maeneo ya vijijini”Alisema Marwa.
Aidha kwa upande wake moja kati ya Raia wa Burundi aliyekamatwa na idara ya uhamiaji Bw,Kajoro Richard alisema sababu ambazo zimekuwa zikisababisha kuingia nchini ni kutokana na ugumu wa maisha nchini mwao na kukosekana kwa ajira.
“Mimi Kweli nilikuja hapa Tanzania nikitokea nchini kwetu Burundi kwa sababu ya kuja kutafuta maisha kwetu ajira ni ngumu sanaa ila naomba wanisamehe nipo tayari kurudi nchini kwetu”Alisema Kajoro.
Naibu kamishina Wilfred Marwa amesema zoezi hilo ni endelevu na kwamba amewataka raia wa kigeni kufuata utaratibu kwa kufuata vibari vya kukaa nchini kwa njia ya halali huku akiwataka watanzania ambao wanaishi na Raia hao kuachana na tabia hiyo na kwamba watakamatwa watafungwa kifungo cha miaka 20 au faini ya milioni ishirini 20.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.