MBOGWE YAPOKEA MBEGU ZA ZAO LA ALIZETI
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe imepokea Mbegu ya Zao la Alizeti Tani 4.84 toka kwa Mamlaka ya Mazao Mchanganyiko (COPRA)ambazo zimegawiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe. Sakina Mohamed kwa Wakulima Wadogo wadogo wa Kata za Masumbwe,Luganga,Nyakafuru Bukandwe na Iponya,ikiwa ni Uzinduzi wa Ugawaji wa Mbegu kwa Wakulima wa Wilaya ya Mbogwe.
Aidha Wilaya inatarajia kupokea Tani 15 za Mbegu za Zao la Alizeti toka Mamlaka hiyo ya Mazao Mchanganyiko (COPRA).
Katika Hafla hiyo ya Ugawaji Mbegu,Mkuu wa Wilaya Mhe. Sakina Mohamed amewaasa Wakulima Wadogo Wadogo Wilayani Mbogwe kuacha kuchukua Mikopo isiyorasmi maarufu kama kausha damu katika kuendesha Shughuli zao za Kilimo ambayo kwa kiasi kikubwa inawaumiza,hivyo amewaasa kuchukua Mikopo katika Taasisi za kifedha zinazotambulika na Serikali hali itakayosaidia kuwa na uhakika wa kufanya Kilimo Chenye tija.
Aidha amewataka Maafisa Kilimo Wilayani humo kutoa Elimu kwa Wakulima juu ya Kilimo cha Alizeti kwa ngazi ya Kijiji na Vitongoji huku akiwasisitiza kutenda haki kwa Wakulima wakati wakutekeleza majukumu yao.
Sambamba na hayo amezitaka taasisi za kifedha kuwafikia Wakulima Wadogo Wadogo na kuwawezesha ili waweze kufanya kilimo Chenye tija.
Hafla hii ya Uzinduzi wa Ugawaji Mbegu za Zao la Alizeti imefanyika leo 17 Januari,2026 katika Ukumbi wa Kagri Uliopo Kata ya Nyakafuru.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.