Leo Februari 4,2026 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ambaye pia ni Mkuu wa idara ya Mipango na Uratibu Ndg. Alex Mang’ara amegawa Vifaa vya Tehama vya Kielimu na Saidizi kwa Walimu wenye Mahitaji Maalumu (Ulemavu wa Viungo).
Vifaa hivyo ambavyo ni Kompyuta Mpakato pamoja na Vishikwambi vitawasaidia Walimu hao kuendelea kutekeleza majukumu Yao ya kufundisha kwa weledi.
Walimu waliopata vifaa hivyo ni kutoka Shule ya Msingi Mkapa, Ilangale pamoja na Nyang’holongo pamoja na Shule ya Sekondari Masumbwe.
Zoezi Hilo limefanyika katika Ofisi za Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbogwe zilizopo kasosobe.
#kazinautu
#tunasongambele
#tabasamulautu
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.