KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI WA MIKOA, HALMASHAURI NA TAASISI ZA OFISI YA RAIS TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Mohamed O. Mchengerwa(Mb) Leo Mei 23, 2025 amefungua Kikao Kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Halmashauri na Taasisi za Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Ukumbi wa Mikutano DodomaJiji ulipo Mji wa Serikali Mtumba.
Katika Kikao Kazi hicho Mhe Mchengerwa amewataka Maafisa Habari Nchini kutoa taarifa sahihi ya yale yanaoyoendelea kwenye maeneo yao.
" Ninyi ni nguzo ya maamuzi ya kuwalisha watanzania ya kile kinachoendelea katika maeneo yenu" Amesema Mhe Mchengerwa (Mb)
Pamoja na hayo Mhe Mchengerwa amewataka Maafisa Habari kuweka Uzalendo mbele katika kuisemea miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika maeneo yao.
Kikao hicho kitaendelea kwa siku mbili ambapo Maafisa Habari kote Nchini wamekutana kuendelea kubadilishana uzoefu namna bora ya kuzitangaza kazi za Serikali katika maeneo yao.
Miongoni mwa Halmashauri zilizoshiriki Kikao Kazi hicho kutoka Mkoa wa Geita ni pamoja na Halmashauri ya Mbogwe,Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Halmashauri ya Wilaya ya Geita,Halmashauri ya Chato na Halmashauri ya Nyang'wale.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.