12 Mei,2025,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mhe. Nsika Sizya ameongoza Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe kukagua Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa Wilayani Mbogwe kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na
1. Ujenzi wa Nyumba ya Watumishi 2 in 1 katika Shule ya Msingi Nyamimbi,kijiji cha Kabanga Kata ya Nhomolwa wenye gharama ya TSH. 92,410,714.29,Fedha toka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) III kupitia Mradi wa TPRP IV (OPEC) Mwaka wa III wa Utekelezaji.
2. Ujenzi wa nyumba ya walimu 2 in 1 katika Shule ya Sekondari Bugegere Kata ya Nyakafuru wenye Gharama ya TSH. 100,000,000/=,Fedha toka SEQUIP.
3. Ujenzi wa Bweni Moja la Wanafunzi 80 katika Shule ya Sekondari Iponya Kata ya Iponya wenye Gharama ya TSH. 130,000,000/=, Fedha toka SERIKALI KUU kupitia Programu ya EP4R.
4. Ujenzi wa Jengo la OPD ngazi ya Zahanati kijiji cha Lubeho Kata ya Nyakafuru wenye Gharama ya TSH. 91,920,539.39/=, Fedha toka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) III kupitia Mradi wa TPRP IV(OPEC) Mwaka wa III wa Utekelezaji.
5. Ujenzi wa Jengo la OPD katika Kituo cha Afya cha Nyakafuru Kata ya Nyakafuru wenye Gharama za TSH. 50,000,000/=, Fedha toka Mapato ya Ndani.
ZIARA ITAENDELEA KESHO TAREHE 13 MEI,2025
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.