DC MBOGWE AKAGUA MIRADI YA BARABARA
Miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara pamoja na madaraja inayotekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Wilayani Mbogwe imeendelea kukaguliwa leo tarehe 19 Januari 2026, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ubora na kwa kuzingatia thamani ya fedha.
Ukaguzi huo umehusisha madaraja, barabara za rami pamoja na barabara za changarawe, miradi inayolenga kuboresha miundombinu ya usafirishaji na kurahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita
Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe
Telephone: +255734412592
Mobile: +255734412592
Email: ded@mbogwedc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.