• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Frequently Asked Questions |
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe

The United Republic of Tanzania MBOGWE DISTRICT COUNCIL MBOGWE DISTRICT COUNCIL

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Administration and human resource
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Finance and Business
      • Social Work
      • Health
      • Ardhi na Mali Asili
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji na Udhibiti Majitaka
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu
    • Units
      • Procurement and Supply
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa na Uwekezaji
  • Huduma
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Hamashauri ya Mbogwe
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu,Afya Na Maji
      • Kamati ya Maaadili
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Bodi ya Ajira
      • Alat Mkoa
      • Kamati ya Vileo
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi(CMAC)
      • Kamati ya Kugawa Ardhi
      • Kamati ya LAVULAK
  • Miradi
    • Project Projection
    • Ongoing Projects
    • Completed Projects
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha za Matukio mbalimbali
  • Machapisho
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Fomu mbalimbali

Halmashauri zaagizwa kutumia mapato yao kwenye huduma za jamii

05 June 2019


Na Mathew Kwembe, Dodoma

Serikali imewaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha kuwa wanaelekeza fedha wanazozikusanya kutoka katika vyanzo vyao mbalimbali katika kuboresha miradi na miundombinu ya jamii ili kuchochea kasi ya maendeleo katika halmashauri zao.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe. Mwita Waitara wakati akiwa katika shule ya sekondari ya Wella iliyopo eneo la Mkonze katika jiji la Dodoma.

Amesema Wakurugenzi wa Halmashauri hawana budi kutumia vizuri mapatao inayoyakusanya kuboresha miradi ya maendeleo kwani serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutatua changamoto na kero mbalimbali kwa jamii.

“Napenda kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri wahakikishe kuwa wanayaelekeza fedha wanazokusanya katika kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili halmashauri zao badala ya kusubiri kero hizo zishughulikiwe na serikali kuu,” amesema.

Naibu Waziri ameongeza kuwa changamoto kama za ukosefu wa matundu ya kutosha ya vyoo, uchakavu wa miundo mbinu ya shule, na kero nyingine za aina hiyo zinaweza kutatuliwa kwa kupitia makusanyo ya halmashauri husika.

Mbali na kutembelea sekondari ya Wella, ambayo imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo za majengo yake yote kutokamilika na upungufu wa matundu ya vyoo, Naibu Waziri pia alitembelea eneo la Dodoma Makulu ambapo alijionea namna kikundi cha vijana cha Jikomboe kinavyojishughulisha na ufyatuaji wa matofali, kikiwa ni miongoni mwa vikundi mbalimbali vilivyopata fedha za mkopo kutoka halmashauri ya jiji la Dodoma.

Pia Mhe Waitara ametembelea eneo la Ipagala na kuona ujenzi wa shule ya mfano unavyoendelea , mradi wa kimkakati wa ujenzi wa soko na stendi  wenye thamani ya shilingi bilioni 34, sekondari ya miyuji kukagua umaliziaji wa vyumba sita vya madarasa, na sekondari ya msalato kukagua ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Dodoma bwana Godwin Kunambi alimweleza Naibu Waziri juu ya mikakati ya jiji hilo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili shuke za msingi na sekondari ambapo amesema kuwa katika bajeti ijayo jiji limetenga kiasi cha shilingi bilioni 8 kutatua changamoto hizo.

Amesema kuanzia sasa jiji la Dodoma litahakikisha kuwa ujenzi wa shule zake utakuwa wa kisasa unaoendana na taswira ya jiji la Dodoma ambapo chini kutawekwa marumaru badala ya sakafu kama ilivyo hivi sasa na juu bati zake zitawekwa rangi kulingana na mpangilio wa ujenzi wa jiji hilo.

Akizungumzia kuhusu changamoto zinazoikabili shule ya sekondari ya wella ambayo majengo yake mengi hayajakamilika licha ya kuanza kutumiwa na walimu na wanafunzi wa shule hiyo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa mwaka huu jiji lilipeleka shilingi milioni 50 kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya miundombinu ya shule na kwamba wanatarajia kuwa katika mwaka ujao wa fedha majengo yote ya shule hiyo yatakarabatiwa kwa kuwekewa marumaru na mabati kupakwa rangi pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.

Katika ziara yake hiyo ambayo ni ya kwanza kutembelea jiji la Dodoma kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, Mhe. Waitara aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mhe.Patrobas Katambi, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma bwana Godwin Kunambi na viongozi mbalimbali kutoka mkoa wa Dodoma na jiji la Dodoma

Announcements

  • Watoto wa kike waliokatisha Masomo yao November 01, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA USAJILI WA ANWANI ZA MAKAZI March 09, 2022
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi kwa Walimu September 06, 2020
  • Ratiba ya Kampeni za Kampeni Jimbo la Mbogwe August 26, 2020
  • View All

Latest News

  • MKUU WA WILAYA SAKINA MOHAMED AMEFANYA KIKAO NA WATUMISHI IDARA YA AFYA WA KITUO CHA AFYA MASUMBWE

    May 15, 2025
  • KAMATI YA FEDHA,UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO MBOGWE

    May 13, 2025
  • KAMATI YA FEDHA YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO MBOGWE

    May 12, 2025
  • WAENDESHA VIFAA VYA BIOMETRIKI NA WAANDISHI WASAIDIZI WAKIPATA MAFUNZO

    April 29, 2025
  • View All

Video

UFUNGUZI WA MAJENGO MAPYA NA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA CHA MASUMBWE, GEITA
More Videos

Quick Links

  • MKOA WA GEITA
  • WIZARA YA TAMISEMI
  • IKULU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  • MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA)
  • BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA(NECTA)
  • WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
  • WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TKNOLOJIA
  • WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Related Links

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora
  • Mkoa wa Geita

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Mbogwe District council ,Masumbwe-Mbogwe,Geita

    Postal Address: P.O Box 1 Masumbwe

    Telephone: +255734412592

    Mobile: +255734412592

    Email: ded@mbogwedc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.